Shakila Nyerere
UMOJA wa wastaafu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi (JWTZ) wamesema hawakubaliani na mpango wa kuanzishwa kwa Mji mpya wa kisasa, Kigamboni jijini Dar es Salaamu, kwa kuwa madai yao ya msingi hayajazikilizwa.
Akizungumza na vyombo vya habari jana, Mwenyekiti wa kikundi hicho, Thadei Mgoso alisema kutokana na kukiukwa kwa utaratibu uliowekwa hawako tayari kukubaliana na mradi wa kuendeleza mji wa Kigamboni.
Mgoso alisema Serikali kupitia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, imekataa kushiriki kwenye midahalo mbalimbali na pia imeshindwa kujibu tuhuma zinazotolewa na wakazi wa kigamboni, kupitia barua na vyombo vya habari.
“Sisi hatujaukataa mradi, lakini wamekosa kutushirikisha katika kila jambo lililokuwa likituhusu na badala yake waliitwa wadau wengine kushiriki vikao hivyo, huu ni ukiukwaji wa sheria kama tulivyokuwa tumekubaliana,” alisema.
Alisema kutokushirikishwa kwa wamiliki wa ardhi katika hatua za kutangazwa kwa mradi, mpango wa jumla, mpango kamili, na kuundwa kwa Mamlaka ya Uendelezaji wa Jiji la kisasa Kigamboni- Kigamboni Develoment Authority-KDA), kumesababisha wakose imani.
Alisema kumekuwapo na ukiukwaji wa sheria na udanganyifu unaofanywa na viongozi mbalimbali na kusababisha wananchi kupoteza imani na serikali.Aliesema miongoni mwa ziara za mara kwa mara zinazofanywa na wageni na matajiri kwenda katika mji huo zimekuwa zikiwatia hofu…soma zaidi www.mwananchi.co.tz
No comments:
Post a Comment