MBUNGE WA CHADEMA MH MSIGWA AKIONGEA NA WANANCHI WA JIMBONI KWAKE.
KAMPENI YA ONDOA CCM DAR KUENDELEA LEO 11/02/2012
Ndugu wananchi ratiba ya ONDOA CCM DAR: KESHO JMOS. JIMBO LA KAWE MAENEO YA TEGETA, JIMBO LA KINONDONI MAENEO YA SUNNA NA JIMBO LA TEMEKE MTONI KWA AZIZI ALLY UTAONA BENDERA BARABARANI ZITAKUPELEKA MPAKA KWENYE MKUTANO.
ILA POLICE WALITAKA KULETA HILA JUU YA MKUTANO WA TEGETA KWA KUTUANDIKIA BARUA YA KUAHIRISHA MKUTANO WETU KWA HOJA YA MASHAMBULIO YA KIGAIDI, ILA NIKAONGEA NA RPC WA KINONDONI BWANA KENYELA NA KISHA TUKAFIKIA MUAFAKA AKATUPATIA KIBALI NA KUFUTA ILE BARUA YAO YA AWALI AMABAYO ILITOKEA KWENYE KITUO KIDOGO CHA KAWE.
WATATUUA KWA RISASI ZA MOTO, WATAKUFA KWA PRESHA YA DHAMBI, AHSANTENI MUNGU YUPO UPANDE WETU NA MSIOGOPE.
HENRY J KILEWO
KATIBU (M) KINONDONI
KANDA YA DAR ES SALAAM
BAADA YA MALIPO YA MADAKTARI NINI TAFSIRI YAKE?
Afisa Uhusiano katika hospitali ya taifa ya Muhimbili Aminieli Eligaesha akizungumza na waandishi wa habari leo Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam (hawapo pichani) kuhusu kurejea kwa huduma za afya katika hospitali hiyo, kufuatia mgomo wa madaktari bingwa na wauguzi uliofanywa katika kipindi cha wiki tatu sasa.
KAMANDA KILEWO AKIFUNGUA MSINGI WA CHAMA JIMBO LA KAWE
Katibu wa chadema mkoa wa kinondoni na Kanda Maalum ya Dar es salaam Bwana Henry Kilewo akifungua msingi wa chama, kamanda aliwatia ujasiri vijana akiwataka kujiandaa kupambana na changamoto mbalimbali zinazowakabili katika maisha, na kutaka wasiongope kufa wakipigania ukweli. kamanda aliendelea kusema Watatuua kwa risasi za moto na wao watakufa kwa presha za dhambi tusiongope mapambana lazima yaendelee… huyo ni kamanda Kilewo, kisha akatuaga na kuelekea Arusha.
WAISLAMU WAANDAMANA
KWA NINI SIKUMSALIMIA JK,DK.SLAA
Fredy Azzah
KATIBU Mkuu wa Chadema Dk Willibrod Slaa amesema kuwa, hakuweza kusalimiana na Rais Jakaya Kikwete kutokana na Jiografia ya eneo la makaburini lilivyopangwa na watu wa usalama wa taifa pamoja na kamati ya mazishi kutomruhusu kufanya hivyo.
KATIBU Mkuu wa Chadema Dk Willibrod Slaa amesema kuwa, hakuweza kusalimiana na Rais Jakaya Kikwete kutokana na Jiografia ya eneo la makaburini lilivyopangwa na watu wa usalama wa taifa pamoja na kamati ya mazishi kutomruhusu kufanya hivyo.
Hata hivyo Dk Slaa alisisitiza kuwa, kwa upande wake, kwenye msiba siyo sehemu ya kwenda kwa ajili ya kusalimiana na watu ama kurekebisha mambo yaliyoharibika bali ni sehemu ya kumwombea marehemu.
“Siyo hulka ya Dk Slaa kutumia misiba kama sehemu ya kusalimiana, wala kutengeza mambo yaliyoharibika, mimi huwa naenda kwenye msiba kwa lengo moja tu la kumwombea marehemu, huwa simtazami hata mtu aliyekaa pembeni yangu,” alisema Dk Slaa alipozungumza kwa njia ya simu jana.
Alifafanua kuwa, katika eneo la makaburi kulikuwa na mabanda matano ambayo yalipangwa kwa ajili ya Askofu, Rais, Viongozi wa vyama vya siasa, mwili wa marehemu na familia na banda jingine lilikuwa la watu wengine waliohudhuria mazishi hayo.
“Sasa kutoka alipokuwa amekaa Rais mpaka kwenye banda nilipokuwa mimi, kulikuwa na umbali wa karibu mita 20, sasa mlitaka nikimbie kumsalimia Rais nivunje protokali kisha nikamatwe na usalama wa taifa,” alisema Dk Slaa. Alisema alikuwa mtu wa kwanza kufika makaburini kwa lengo la kuangalia jinsi kaburi la mbunge wa chama chake lilivyochimbwa kisha akaonyeshwa sehemu ya kukaa na watu wa usalama wa taifa.
Alisema kuwa, hata katika wakati wa kuaga mwili wa Marehemu Regia Mtema, katika ukumbi wa Karejee, kulikuwa na utaratibu kama huo ambapo ilitengwa sehemu ya kukaa Makamu wa Rais, Spika wa Bunge, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani na Makamu wake na yeye Dk Slaa akawekewa sehemu yake kama Katibu wa Chama alichokuwa akikitumika marehemu.
“Mimi sipendi kuweka siasa kwenye mambo kama ya msiba, Dk Slaa siyo kichaa siyo kichaa aanze kukimbia kumsalimia Rais. Katika sehemu kama ile Rais huwa anakuja baada ya watu wote wakiwa wameshakaa, yeye ndiye hupita na kuanza kusalimia watu na hamjaona hata sehemu moja aliponyoosha mkono kunisalimia nikamkwepa,” alisema Dk Slaa:
“Msiba siyo mahali pa kutengeza urafiki, au kutengeza mambo yaliyo haribika, pale ni ibada tu na kumuombea marehemu siyo sehemu ya kufanya siasa” alisisitiza Dk Slaa. Jana baadhi ya vyombo vya habari viliripoti kuwa, Dk Slaa alishindwa kusalimiana na Rais Jakaya Kikwete katika mazishi ya Regia Mtema yaliyofanyika kijijini kwao Ipangalala Morogoro juzi.Regia alifariki dunia Januari 14 kwa ajali ya gari iliyotokea katika eneo la Ruvu mkoani Pwani. Chanzo: gazeti Mwananchi.
Harakati zinaendelea sio ! vizuri
ReplyDelete